Imewekwa: 25 Apr, 2025

Katika sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Veterinari Duniani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na chama cha madaktari wa wanyama Tanzania(TVA) wametoa huduma za afya ya wanyama katika Halmashauri za Wilaya na Mji Mbulu, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Halmashauri za Wilaya na Mji Babati.
Huduma hizo zimeanza leo Aprili 24-26, 2025 ambapo mbali na huduma hiyo ya kukinga wanyama dhidi ya magonjwa wameendelea kutoa elimu kwa wafugaji hao kuhusu ugonjwa wa kichaa cha mbwa na huduma hizo zote zinatolewa bila malipo katika maeneo mbalimbali yaliyo ainishwa.
Pamoja na shughuli hizo wataam hao wameandaa maonyesho makubwa yanayo endelea katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa mjini Babati.