Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania na Sekretarieti ya Baraza, ninayofuraha kuwakaribisha katika tovuti yetu, ambayo imetengenezwa kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu shughuli zinazofanywa na Baraza la Veterinari Tanzania katika kusimamia taaluma ya Veterinari na kuboresha utoaji wa huduma za afya ya wanyama nchini.

 

Ni imani yangu kuwa tovuti hii itakuwa nyenzo sahihi itakayoiwezesha Wataalamu na wananchi kwa ujumla kupata habari na elimu kupitia nyaraka,ambapo nyaraka mbalimbali kama vile Sheria ya Veterinari (SURA 319) na Kanuni na Miongozo yake, zinapatikana kwa urahisi.

 

Wakati tunatekeleza majukumu yetu ya msingi kama ilivyoainishwa chini ya Kifungu cha 5(1) (2) cha Sheria ya Veterinari Sura ya 319 ya Sheria za Tanzania, tumedhamiria kuhakikisha kuwa wadau wetu na wananchi kwa ujumla wanapata taarifa muhimu kwa wakati.

 

Mwisho,lakini si kwa umuhimu ninatoa wito kwa wadau kutembelea tovuti yetu mara kwa mara na kuwasiliana nasi kwa maelezo yoyote ya ziada yanayohitajika kwa ajili ya ufafanuzi zaidi juu ya hududma zetu au maoni,ushauri kwa ajili ya uboreshaji.

 

Karibu sana.

 

Dkt AMANI J. KILEMILE

MSAJILI